Field Misheni Tanga - Tanzania
Huduma ya Jesus Glory (JG) kupitia Kufika Kusikofikiwa na Injili Ya Yesu Kristo (KKI) inatarajia kufanya misheni mkoani Tanga katika vijiji vya Mlola na Hemtoe kuanzia tarehe 01/06/2021, Lengo ni kufikisha injili vijijini na kuokoa watu kwa jina la Yesu. Tunaomba mchango wako wa hali na mali katika kufanikisha misheni hii katika kuhubiri Injili na Mungu akubariki sana. Tuma sadaka yako kupitia namba 0752 883 573 au 0753 885 118 zenye jina JESUS GLORY. Misheni hii itahusisha kuhubiri Injili, Ushuhudiaji wa nyumba kwa nyumba,Mkutano na sinema.



