Safari ya kuelekea Songwe ilianza siku ya jumamosi , natulifika saa 6:30 usiku katika kijiji cha Muwawa . Tulipokelewa na mwenyekiti wa kijiji Msafu ambaye ndiye aliyekuwa mwenyeji wetu, pia tulilala nyumbani kwake. Tarehe 21/02/2021 siku ya Jumapili tulielekea Nyenjele kuwakaribisha wachungaji kwenye mkutano; tulifanikiwa kuwapata wachungaji saba ila waliofika kwenye mkutano walikuwa ni wachungaji sita na wa saba alitoa udhuru hakufika.Siku hii ya jumapili pia tulifanikiwa kukutana na viongozi wa serikali ambao tulifanikiwa kujadiliana mambo mbalimbali yanahusu injili, mkutanao ulifanikiwa sana na kwa matokeo mazuri tulikubaliana kwamba mkutano utafanyika mwezi wa tano na wachungaji walikubali kutuandalia malazi na chakula . Viwanja vya mkutano viongozi wa serikali walikubali kutoa eneo.Taasisi itakodisha vyombo, sinema, jukwaa, kusafirisha Wainjilisti kutoka mkoa mmoja kwenda sehemu ya mkutano pia kituo kitakuwa kimoja katika kijiji cha Muwawa na Nyenjele kituo ni kimoja tu. Changamoto zilizopo ni watu wa kijiji kutokuhudhuria kwenye neon la Mungu, makanisa machache na yako mbali na maeneo wanakoishi hivyo kuwafanya watu kuona kwmba injli ni kitu kigeni kwao na kuwafanya waabudu mila na desturi na miungu ya kwao kwani makanisa yaliyopo ni Moraviani, Romani katoliki na Africani ambayo haya yalikuwa yametangulia kuwepo katika kijiji cha Nyenjele, Wababa na wamama wote ni walevi hawafanyi kazi hivyo kusababisha hata watoto wao kutoenda shule na na kuanza kunywa pombe wakiwa wadogo, ujambazi umekithiri sana katika kijiji cha Nyenjele. Ombi la wachungaji na viongozi wa serikali wanaomba Taasisi iwajengee shule ya neno la Mungu ili watoto wao waweze kupata Elimu ya neno la Mungu ili kuweza kuponya kizazi kilichopo na mambo mabaya yanayowaharibu kiakili na kimaadili. Katika kufanikisha jambo hilo Serikali imeahidi kutoa eneo la ujenzi na wachungaji nao waliahidi kutoa matofali ili kukamilisha mradi huo. Gharama tulizotumia kwnye safari ni jumla ya 520,000 ambayo iliyojumlisha chakula malazi na nauli kwa safari nzima. Viongozi wa maandalizi ya mkutano mwezi mei ni Bahati M. Nyenjela – Mwenyekiti TAG 0765 153 940 Derick T. Sihangwe –Katibu African 0767 493 936 Binisenti Silozi – Mwenyekiti Maombi 0763 209 726 Elda S. Mbeyla- Mw/K Msaidizi Maombi 0759 202 868. Tulimaliza mambo yote yanayohusu maandalizi ya Misheni mwezi Mei siku ya Jumatatu tarehe 22/02/2021 na kesho yake siku ya Jumanne tarehe 23/02/2021 tulianza safari ya kurudi Dar es Salaam ambapo tuwasili jijini Dar es Salaam saa 8.30 usiku. Mwisho tunamshukuru Mungu kwa kutulinda na kutuongoza, kwani tulisafiri salama. Pia tunashukuru huduma nzima ya Jesus Glory kwa maombi yao kwetu, shukrani za kipekee ziende kwa Mkurugenzi mkuu kwa kuwa pamoja na sisi, kutufwatilia hatua kwa hatua tangu tulivyoanza safari mpaka kurudi hakutuacha hata tatua moja. Mungu ambariki sana.
Vivamus convallis
Integer faucibus magna vitae augue suscipit a varius sem scelerisque. Nunc scelerisque tempus nunc in euismod. In sagittis congue sodales. Cras sit amet est nibh. Suspendisse eget ligula in nulla iaculis interdum nec a odio. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Cras massa odio, facilisis tincidunt blandit semper, lacinia semper dui. Donec viverra eros quis urna congue facilisis. Vivamus convallis imperdiet porta. Aliquam a nisi risus, vitae faucibus sem.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Nulla convallis egestas rhoncus. Donec facilisis fermentum sem, ac viverra ante luctus vel. Donec vel mauris quam. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Nulla convallis egestas rhoncus. Donec facilisis fermentum sem, ac viverra ante luctus vel. Donec vel mauris quam.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Nulla convallis egestas rhoncus.
